Jina  la kitabu/ Tittle of Book: Mwongozo Wa Ufugaji Bora  Wa  Nyuki

Jina la Mwandishi:  Pius B. Ngeze

ISBN  :978   9987   07   060   2

Bei: 15,000/=

Mwaka  wa Uchapishaji /Year of Publication: 2017

 Maelezo mafupi /Brief summary

Inakadiriwa kuwa nchi hii ina rasilimali za ufugaji wa nyuki zenye uwezo wa kuzalisha mazao ya nyuki kufikia takribani tani 138,000 za asali na tani 9,200 za nta kwa mwaka.

Lakini, kwa mwaka 2016, wastani wa uzalishaji ni tani 5,600 za asali zenye thamani ya shilingi bilioni 14.5 na tani 379 za nta zenye thamani ya shilingi bilioni 1.04

ambazo huzalishwa kwa mwaka.Hii ni sawa na asilimia tano (5) tu ya uwezo wa uzalishaji. Kati ya tani 5,600 za asali zinazozalishwa, ni tani 477 tu zinazosafirishwa kwenda nje ya nchi,

ambazo ni sawa na asilimia kumi na moja (11) ya asali inayozalishwa nchini. Kiasi chote cha nta inayozalishwa huuzwa nchi za nje. Mahitaji ya asali na nta ndani na nje ya nchi yetu

ni makubwa sana na hatuwezi kuyatosheleza. Tatizo ni uzalishaji na si soko. Soko lipo, ni kubwa sana na  endelevu. Aidha, bei kwa asali bora ni kubwa sana. 

 

Kitabu hiki kitasaidia walengwa ambao ni wafugaji wa sasa na wafugaji watarajiwa wa nyuki kuzalisha asali na anta nyingi na iliyo bora kwa kila mzinga kwa

kuendesha Ufugaji Bora wa Nyuki badala ya kuendelea kutegemea ufugaji wa kiasili ili kutumia kikamilifu rasilimali za ufugaji zilizopo nchini.