Jina la Kitabu:Mwongozo wa Kilimo Bora cha Kahawa

Mwandishi/Author:Pius B. Ngeze

ISBN:78   9987   426  31    7  

Bei/Price: 25,000/=

Kiwango/Level:Watu wazima/Adults

Lugha/Language:Kiswahili

Mwaka wa Uchapishaji:2016

Maelezo mafupi:

Mwongozo wa Kilimo Bora cha Kahawa ni kitabu chenye Sura 23  zinazohusu  maeneo  tofauti  ya  kilimo  bora  cha  zao   hili muhimu nchini ambayo ni pamoja na:

• Vikwazo vya uzalishaji. 

• Kanuni za kilimo bora.

• Ukuzaji wa miche inayotokana na mbegu na vipingili.

• Utayarishaji wa shamba.

• Upandikizaji  wa miche shambani.

• Ukarabati wa shamba la zamani lililokanda.

• Mbadilisho wa mzunguko wa kahawa shambani.

• Upogoleaji na utengenezaji wa umbo la mbuni.

• Rutuba ya udongo, lishe ya mibuni, na matumizi ya Mbolea.

• Upandaji  na  utunzaji  wa  miti  ya  kivuli  katika  shamba  la 

   kahawa.

• Umwagiliaji wa shamba la kahawa.

• Udhibit wa magugu, wadudu na magonjwa.    

• Ufanisi na tahadhari katika kutumia na kuhifadhi viuatilifu.

• Uchumaji na utayarishaji wa kahawa.

• Utengaji wa kahawa safi katika madaraja.

• Ladha ya kahawa na uonjaji.

• Utunzaji wa kumbukumbu.

Kitabu hiki kimeandaliwa mahsusi kwa ajili ya Wakulima wapya na wa zamani wa  kahawa,  Maofisa Ugani,  Maofisa  Kilimo,  na Maofisa na Viongozi wa Vitongoji, Mtaa,  Vijiji, Kata,  Tarafa  na Wilaya.

Ni   matumaini  yetu  kuwa  elimu   iliyomo  itasaidia  kuongeza

uzalishaji na ubora wa kahawa nchini.