Change Language
TEPU Downloads
User Options

Order Book at: $8, Tshs 20,000/=  


You can Read this Book at:


Tshs 5000/- to MPESA   


Tshs 5000/- to AIRTEL MONEY  


Tshs 5000/- to TIGO PESA  


$4 MASTERCARD/VISA-CARD  


BRIEF BOOK SUMMARY:
Riwaya hii inaudurusu na kuzulu uhuru na dhima nzima ya kuwa huru. Inaona shaka na uhuru wa baadhi ya nchi barani Africa unaowanufaisha watawala waliojigeuza miungu pamwe na walamba viatu wao. Watu wa kawaida hawaruhusiwi kutia mkono kwenye deste nao wale halua! Riwaya hii inahimiza wengi au umma kushika hatamu. Inashadidisha umma uutathimini na kuuhoji upya uhuru wanaoambiwa ni wao. Wakati si wao. Katika kufanikisha hili, tofauti na mapambano yam tutu wa bunduki, mauaji na ghasia, riwaya hii inawahimiza waathirika waishio kwa matumaini kuupigania na kuupata uhuru wa kweli kupitia kwenye sanduku la kura. Riwaya inahimiza watawaliwa kuhakikisha wanawawajibisha watawala kama sehemu ya uwajibikaji wao. Kila mmja awajibike kwa mwenzake. Inawataka watawala wawatumikie watawaliwa badala ya kuwatumia kama punda kwa kuwabeba wao na mizigo yao. Riwaya inapinga ufisi, ukuku,umbwa, ukondoo, usindano,ukijiko,na tabia nyingine kama hizo; inasajihisha usimba , umizani, na utambuzi, utendaji na ulinzi wa haki. Hapo ndipo utamwona mhusika mkuu, mzee Njema, akipambana na uongozi mbovu kuanzia kijijini mwake hadi wilaya nam hatimaye, taifa. Cheche ya shujaa inawasha moto unaouamsha na kuugengeua umma kiasi cha kuangusha serikali dhalimu ya Mizengwe kupitia sanduku la kura.