Change Language
TEPU Downloads
User Options

Order Book at: $8, Tshs 19,000/=  


You can Read this Book at:


Tshs 10000/- to MPESA   


Tshs 10000/- to AIRTEL MONEY  


Tshs 10000/- to TIGO PESA  


$4 MASTERCARD/VISA-CARD  


BRIEF BOOK SUMMARY:
Lugha ni chombo cha mawasiliano. Lugha hutumika kama njia muhimu ya mawasiliano kwa shughuli mbalimbali zinazoihusu jamii inayohusika. Kutokana na umuhimu huu, Kiswahili imekuwa kikifundishwa kama somo shuleni na vyuoni. Aidha, watu wazima hujifundisha au hufundishwa Kiswahili katika nchi mbalimbali duniani. Kwa misingi hii kitabu hiki kimeandaliwa mahususi ili kiwasaidie wanafunzi na watu wengine wanaohitaji kuimarisha au kupanua ujuzi wao lugha hii. Kitabu hiki ni mwongozo imara kwa wanafunzi na watu wengine wanaotaka kuinua kiwango cha uelewa wao wa Kiswahili. Kitabu kina jumla ya sura nane ambazo zinazingatia utaratibu maalumu ufuatao: Sura ya Kwanza ni Ufahamu; Sura ya Pili inahusu Utungaji; Sura ya Tatu imechambua vipengele vya Sarufi; Sura ya Nne inaelezea juu ya Methali na Misemo inayotumika katika lugha ya Kiswahili. Sura ya Tano inachunguza Mbinu za Kiswahili; Sura ya Sita ni Majibu ya Mazoezi na Msamiati. Majibu hayo ni kwa baadhi ya mazoezi yaliyotolewa kitabuni. Aidha, sura hiyo pia inaonyesha orodha ya Msamiati na fasiri yake; Sura ya Saba ni Mitihani ya kujipima au kupima uelewa wa msomaji na Sura ya Nane ni Majibu ya Mitihani hiyo. Misingi na kanuni bora katika kila mada zimechambuliwa kwa kina. Aidha, kitabu hakimlazimishi mwanafunzi kutegemea msaidizi bali mwalimu mkubwa ni kitabu chenyewe. kwa wanafunzi na watu wote wanaotaka kujifunza na kuhitimu Kiswahili.